Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu

WCF Logo
Vitengo

KITENGO CHA UKAGUZI WA NDANI

Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani ni kitengo kilichoanzishwa ili kumsaidia Afisa Masuuli katika kutimiza malengo ya Taasisi. Sheria ya Fedha za Umma ya mwaka 2004 iliyorekebishwa mwaka 2010 inawapa Wakaguzi wa Ndani jukumu la kuchunguza na kutathmini utoshelevu na ufanisi wa udhibiti wa ndani, udhibiti wa  Vihatarishi na maswala ya utawala katika mashirika.

Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani kinafanya kazi zifuatazo:-

  • Kumshauri Afisa Masuuli kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu utendaji wa majukumu ya Taasisi pamoja na usimamizi mzuri wa rasilimali na kupunguza vihatarishi katika Taasisi;
  • Kuandaa taarifa za ukaguzi wa ndani za kila robo mwaka kwa ajili ya  menejimenti
  • Kufanya ukaguzi wa ufanisi kwa kupitia taarifa za utendaji za kila robo mwaka za Idara na kutoa mwongozo unaofaa;
  • Kuandaa mpango wa ukaguzi wa ndani unaozingatia viatarishi na mpango mkakati wa ukaguzi wa ndani na kuwasilisha katika Kamati ya Ukaguzi ya Taasisi kwa ajili ya kuidhinishwa;
  • Kutoa taarifa ya ukaguzi ikijumuisha mapendekezo ya uboreshaji wa udhibiti wa ndani ili kulinda rasilimali na kukuza ukuaji wa Taasisi;
  • Kuijulisha Kamati ya Ukaguzi kuhusu mwenendo na ufanisi katika ukaguzi wa ndani;
  • Kusaidia katika uchunguzi wa matukio makubwa yanayoshukiwa kuwa ya udanganyifu ndani ya Taasisi na kuiarifu menejimenti na Kamati ya Ukaguzi;
  • Kuzingatia wigo wa kazi ya Wakaguzi wa Nje, kama inavyofaa, kwa madhumuni ya kutoa huduma bora ya ukaguzi kwa Taasisi kwa gharama inayokubalika;
  • Kupitia na kutoa taarifa juu ya udhibiti sahihi wa mapato, uhifadhi na matumizi ya rasilimali fedha za Taasisi;
  • Kupitia na kutoa taarifa juu ya ufuataji wa taratibu za fedha na uendeshaji zilizowekwa katika sheria yoyote au kanuni au maelekezo yoyote ya udhibiti wa mapato na matumizi ya Taasisi;
  • Kupitia na kutoa taarifa juu ya uainishaji na mgawanyo sahihi wa akaunti za mapato na matumizi;
  • Kuandaa taratibu za ukaguzi ili kuwezesha kufuata viwango vya kimataifa;
  • Kufuatilia na kuhakikisha kuwa taratibu za kifedha zinazingatia kanuni, sera na taratibu za fedha za Taasisi;
  • Kuhakikisha kwamba wakuu wa Idara na Vitengo na Sehemu wanahifadhi orodha ya mali zote zinazohamishika na zisizohamishika kwa mujibu wa sera na kanuni za Taasisi;
  • Kukuza uhusiano mzuri na wakaguzi wa nje;
  • Kutoa taarifa kwa uongozi kuhusu tukio lolote linaloshukiwa la kukosa uaminifu;
  • Kushauri menejimenti  juu ya hitaji la kuhuisha au kubadilisha miongozo ya sera na taratibu za kifedha; na
  • Kufanya kazi yoyote inayohusiana na ukaguzi kama itakavyoagizwa na Mkurugenzi Mkuu.