Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu

WCF Logo
UTOAJI WA RUZUKU YA MBEGU ZA MAHINDI ZILIZOTHIBITISHWA UBORA KATIKA MSIMU WA MWAKA 2024/2025
04 Sep, 2024 Pakua

Katika msimu wa 2024/2025, Serikali imepanga kutoa ruzuku ya mbegu za mahindi zilizothibitishwa ubora (certified seeds) katika mikoa yote yenye fursa ya uzalishaji wa zao hilo. Katika utekelezaji wa mpango huo, Wizara ya Kilimo imeiteua Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) kuratibu utekelezaji wa mpango huo ikiwa ni pamoja na kusajili makampuni ya mbegu na mawakala watakaohusika katika mpango huu wa ruzuku ya mbegu za mahindi.