Control Plots
Control Plots
Maana ya Jaribio la Uhalisia wa aina za mbegu zilizo katika uzalishaji
Hili ni jaribio la kukagua sifa na uhalisia wa kitabia (genetic purity) wa mbegu katika hatua mbali mbali za uzalishaji. Jaribio hili lina madhumuni yafuatayo
Madhumuni na umuhim wa jaribio
- Kuthibitisha ikiwa sampuli ya aina mpya za mbegu iliyoko katika uzalishaji bado ina sifa linganishi (description) kwa aina ya mbegu hiyo na hivyo kuthibitika ubora wake.
- Kuhakikisha endapo sampuli ya aina mpya ya mbegu husika bado ina viwango katika sifa za usafi wa kitabia(genetic purity)
Namna jaribio linavyofanyika
- TOSCI huchukua Sampuli mbali mbali za aina za mbegu katika madaraja tofauti wakati wa zoezi la uthibiti ubora wa mbegu. Sampuli hizi huchukuliwa kutoka kwa wazalishaji/wagunduzi wa mbegu ambao ni makampuni binafsi na taasisi za serikali zinazojihusisha na masuala ya mbegu.
- Sampuli hizo hupandwa katika eneo la majaribio kwa kila msimu
- Takwimu za sifa za mwonekano huchukuliwa katika kila hatua ya ukuaji wa mimea ikiwa shambani.
- Takwimu hizo hulinganishwa na sifa ya msingi ya aina hiyo ya mbegu ili kubaini endapo kuna utofauti
- Endapo kuna utofauti uliobainishwa TOSCI inaweza kuwaita wazalishaji/wagunduzi wa aina hiyo ili kutoa mapendezo na
- Viwango wa utafauti vilivyogundulika hutathiminiwa ili kuchukua hatua dhidhi ya aina ya mbegu ambayo itagundulika kupoteza uhalisia wake.